Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi katika mkono wangu wa kulia, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako?
Mathayo 22:45 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, ikiwa Daudi anamwita Kristo ‘Bwana,’ anawezaje kuwa mwanawe?” Biblia Habari Njema - BHND Basi, ikiwa Daudi anamwita Kristo ‘Bwana,’ anawezaje kuwa mwanawe?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, ikiwa Daudi anamwita Kristo ‘Bwana,’ anawezaje kuwa mwanawe?” Neno: Bibilia Takatifu Kama basi Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ awezaje kuwa mwanawe?” Neno: Maandiko Matakatifu Kama basi Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ awezaje kuwa mwanawe?” BIBLIA KISWAHILI Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe? |
Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi katika mkono wangu wa kulia, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako?
Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu yeyote tangu siku ile kumwuliza neno tena.
ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele. Amina.
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulikana kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,
Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzawa wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.