nasi tutakata miti katika Lebanoni, kadiri utakavyohitaji; na kukuletea tukiieleza baharini mpaka Yafa; nawe utaipeleka Yerusalemu.
Matendo 9:42 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ikajulikana katika mji mzima wa Yafa; watu wengi wakamwamini Bwana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Habari za tukio hili zilienea kila mahali huko Yopa, na watu wengi wakamwamini Bwana. Biblia Habari Njema - BHND Habari za tukio hili zilienea kila mahali huko Yopa, na watu wengi wakamwamini Bwana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Habari za tukio hili zilienea kila mahali huko Yopa, na watu wengi wakamwamini Bwana. Neno: Bibilia Takatifu Habari hizi zikajulikana sehemu zote za Yafa na watu wengi wakamwamini Bwana Isa. Neno: Maandiko Matakatifu Habari hizi zikajulikana sehemu zote za Yafa na watu wengi wakamwamini Bwana Isa. BIBLIA KISWAHILI Ikajulikana katika mji mzima wa Yafa; watu wengi wakamwamini Bwana. |
nasi tutakata miti katika Lebanoni, kadiri utakavyohitaji; na kukuletea tukiieleza baharini mpaka Yafa; nawe utaipeleka Yerusalemu.
Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa BWANA; akateremka hadi Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akalipa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa BWANA.
Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo.
Basi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini.
Naye Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenituma.
akatueleza jinsi alivyomwona malaika aliyesimama nyumbani mwake na kumwambia, Tuma watu kwenda Yafa ukamwite Simoni aitwaye Petro,
Nilikuwa katika mji wa Yafa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kinashuka, kama nguo kubwa inateremshwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikia.
Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa.
Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi waliosikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Njoo kwetu pasipo kukawia.
Basi Petro akakaa siku kadhaa huko Yafa, nyumbani mwa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi.