Matendo 8:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC akawa akirudi nyumbani, akiwa ameketi garini mwake akisoma kitabu cha nabii Isaya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alipokuwa anasafiri, alikuwa akijisomea kitabu cha nabii Isaya. Biblia Habari Njema - BHND Alipokuwa anasafiri, alikuwa akijisomea kitabu cha nabii Isaya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alipokuwa anasafiri, alikuwa akijisomea kitabu cha nabii Isaya. Neno: Bibilia Takatifu naye akiwa njiani kurudi nyumbani alikuwa ameketi kwenye gari lake la vita akisoma kitabu cha nabii Isaya. Neno: Maandiko Matakatifu naye akiwa njiani kurudi nyumbani alikuwa ameketi garini mwake akisoma kitabu cha nabii Isaya. BIBLIA KISWAHILI akawa akirudi nyumbani, akiwa ameketi garini mwake akisoma kitabu cha nabii Isaya. |
Haya ni maono ya Isaya, mwana wa Amozi aliyoyaona kuhusu Yuda na Yerusalemu, siku za Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda.
kama ilivyoandikwa katika kitabu cha maneno ya nabii Isaya; Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
Na walipokuwa hawapatani wao kwa wao, wakaenda zao, Paulo alipokwisha kusema neno hili moja, ya kwamba, Roho Mtakatifu alinena vema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya,
Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyesimamia hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu,
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda kulingana na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.