BWANA akamwambia Musa, Mtwae Yoshua, mwana wa Nuni, mtu ambaye roho iko ndani yake, ukamwekee mkono wako;
Matendo 8:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Petro na Yohane wakawawekea mikono hao waumini, nao wakampokea Roho Mtakatifu. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Petro na Yohane wakawawekea mikono hao waumini, nao wakampokea Roho Mtakatifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Petro na Yohane wakawawekea mikono hao waumini, nao wakampokea Roho Mtakatifu. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Petro na Yohana wakaweka mikono yao juu ya wale waliobatizwa, nao wakapokea Roho wa Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Petro na Yohana wakaweka mikono yao juu ya wale waliobatizwa, nao wakapokea Roho wa Mwenyezi Mungu. BIBLIA KISWAHILI Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu. |
BWANA akamwambia Musa, Mtwae Yoshua, mwana wa Nuni, mtu ambaye roho iko ndani yake, ukamwekee mkono wako;
nawe utawaleta Walawi mbele za BWANA; kisha wana wa Israeli wataweka mikono yao juu ya Walawi;
akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yuko karibu kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi.
Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.
Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.
Wakati Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema,
Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.
Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono na wazee.
Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi.
Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu.
na wa mafundisho ya ubatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele.