Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.
Matendo 8:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walipofika waliwaombea hao waumini ili wampokee Roho Mtakatifu; Biblia Habari Njema - BHND Walipofika waliwaombea hao waumini ili wampokee Roho Mtakatifu; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walipofika waliwaombea hao waumini ili wampokee Roho Mtakatifu; Neno: Bibilia Takatifu Nao walipofika wakawaombea ili wampokee Roho Mtakatifu wa Mungu, Neno: Maandiko Matakatifu Nao walipofika wakawaombea ili wampokee Roho wa Mwenyezi Mungu, BIBLIA KISWAHILI ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu; |
Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.
akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.
Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Maana najua ya kuwa haya yatanigeukia kuwa wokovu wangu, kwa sababu ya kuomba kwenu, na kuruzukiwa Roho wa Yesu Kristo;