Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu, nacho kiti cha enzi cha ufalme wake nitakiimarisha milele.
Matendo 7:47 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini Sulemani alimjengea nyumba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Solomoni ndiye aliyemjengea Mungu nyumba. Biblia Habari Njema - BHND Lakini Solomoni ndiye aliyemjengea Mungu nyumba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Solomoni ndiye aliyemjengea Mungu nyumba. Neno: Bibilia Takatifu Lakini Sulemani ndiye aliyemjengea Mungu nyumba. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini alikuwa Sulemani ndiye alimjengea Mwenyezi Mungu nyumba. BIBLIA KISWAHILI Lakini Sulemani alimjengea nyumba. |
Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu, nacho kiti cha enzi cha ufalme wake nitakiimarisha milele.
Ndipo Hiramu, mfalme wa Tiro, akawatuma watumishi wake kwa Sulemani; kwani alikuwa amesikia ya kwamba wamemtia mafuta awe mfalme mahali pa baba yake. Kwa maana Hiramu alikuwa akimpenda Daudi siku zote.
Ikawa katika mwaka wa mia nne na themanini baada ya wana wa Israeli kutoka nchini Misri, katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Sulemani juu ya Israeli, katika mwezi wa Zivu, ndio mwezi wa pili, akaanza kuijenga nyumba ya BWANA.
Basi BWANA amelitimiza neno lile alilolinena; nami nimesimama mahali pa Daudi baba yangu, na kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli, kama BWANA alivyoahidi, nami nimeijenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli.
Ikawa, Daudi alipokuwa akikaa nyumbani mwake, Daudi akamwambia nabii Nathani, Angalia, mimi ninakaa katika nyumba ya mwerezi, bali sanduku la Agano la BWANA linakaa chini ya mapazia.
Ndipo Sulemani akaanza kuijenga nyumba ya BWANA huko Yerusalemu, juu ya mlima Moria, pale BWANA alipomtokea Daudi babaye alipotengeza mahali pale alipoagiza Daudi, katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi.