Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Matendo 7:39 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Mtu huyo baba zetu hawakutaka kumtii, bali wakamsukumia mbali, na kwa mioyo yao wakarejea Misri,

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Lakini yeye ndiye babu zetu waliyekataa kumsikiliza; walimsukuma kando, wakatamani kurudi Misri.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Lakini yeye ndiye babu zetu waliyekataa kumsikiliza; walimsukuma kando, wakatamani kurudi Misri.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Lakini yeye ndiye babu zetu waliyekataa kumsikiliza; walimsukuma kando, wakatamani kurudi Misri.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“Lakini baba zetu walikataa kumtii Musa, badala yake wakamkataa na kuielekeza mioyo yao Misri tena.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“Lakini baba zetu walikataa kumtii Musa, badala yake wakamkataa na kuielekeza mioyo yao Misri tena.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Mtu huyo baba zetu hawakutaka kumtii, bali wakamsukumia mbali, na kwa mioyo yao wakarejea Misri,

Tazama sura
Tafsiri zingine

Matendo 7:39
15 Marejeleo ya Msalaba  

Hivyo Sulemani akamtoa Abiathari asiwe kuhani wa BWANA; ili alitimize neno la BWANA, alilonena juu ya nyumba ya Eli katika Shilo.

Wakamhusudu Musa kambini, Na Haruni, mtakatifu wa BWANA.

wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa BWANA katika nchi ya Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua kwa njaa kusanyiko hili lote.

Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung'unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu?

Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu;

Watu wakamnung'unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu.

Lakini yeye aliyemdhulumu mwenziwe akamsukumia mbali, akisema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu na mwamuzi juu yetu?

Na roho za manabii huwatii manabii.

Mkewe huyo Gileadi akamzalia wana; na hao wana wa mkewe hapo walipokuwa wakubwa wakamtoa Yeftha, na kumwambia, Wewe hutarithi katika nyumba ya baba yetu; kwa sababu wewe u mwana wa mwanamke mwingine.