Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa wagonjwa, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.
Matendo 28:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yalipokwisha kutendeka hayo wengine waliokuwa na magonjwa katika kisiwa wakaja wakaponywa; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kutokana na tukio hilo, wagonjwa wote katika kile kisiwa walikuja wakaponywa. Biblia Habari Njema - BHND Kutokana na tukio hilo, wagonjwa wote katika kile kisiwa walikuja wakaponywa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kutokana na tukio hilo, wagonjwa wote katika kile kisiwa walikuja wakaponywa. Neno: Bibilia Takatifu Jambo hili lilipotukia, watu wote wa kisiwa kile waliokuwa wagonjwa wakaja, nao wakaponywa. Neno: Maandiko Matakatifu Jambo hili lilipotukia, watu wote wa kisiwa kile waliokuwa wagonjwa wakaja, nao wakaponywa. BIBLIA KISWAHILI Yalipokwisha kutendeka hayo wengine waliokuwa na magonjwa katika kisiwa wakaja wakaponywa; |
Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa wagonjwa, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.
Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu;
nao wakatuheshimu kwa heshima nyingi; basi tulipoabiri wakatupakilia vitu vile tulivyokuwa na haja navyo.
Ikawa babake Publio alikuwa akiugua homa na kuhara damu. Paulo akaingia kwake, akaomba, akaweka mikono yake juu yake, na kumponya.
Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani;
hata ikawa katika njia kuu hutoa nje wagonjwa, na kuwaweka juu ya mikeka na magodoro, ili Petro akija, ngawa kivuli chake kimwangukie mmojawapo wao.