Yule bwana akamsifu wakili asiyemwaminifu kwa vile alivyotenda kwa busara; kwa kuwa wana wa ulimwengu huu katika kizazi chao wenyewe huwa na busara kuliko wana wa nuru.
Matendo 27:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi askari wakazikata kamba za mashua, wakaiacha ianguke. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo wale askari walizikata kamba zilizokuwa zimeshikilia ule mtumbwi, wakauacha uchukuliwe na maji. Biblia Habari Njema - BHND Hapo wale askari walizikata kamba zilizokuwa zimeshikilia ule mtumbwi, wakauacha uchukuliwe na maji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo wale askari walizikata kamba zilizokuwa zimeshikilia ule mtumbwi, wakauacha uchukuliwe na maji. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo basi wale askari wakakata kamba zilizoshikilia ile mashua ya kuokolea watu kwenye meli, wakaiacha ianguke humo baharini. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo basi wale askari wakakata kamba zilizoshikilia ile mashua ya kuokolea watu kwenye meli, wakaiacha ianguke humo baharini. BIBLIA KISWAHILI Basi askari wakazikata kamba za mashua, wakaiacha ianguke. |
Yule bwana akamsifu wakili asiyemwaminifu kwa vile alivyotenda kwa busara; kwa kuwa wana wa ulimwengu huu katika kizazi chao wenyewe huwa na busara kuliko wana wa nuru.
Akasokota kikoto cha kamba, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng'ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;
Na kulipokuwa kukipambazuka Paulo akawasihi wote wale chakula, akisema, Leo ni siku ya kumi na nne kungoja na kufunga, hamkula kitu chochote.