Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Matendo 24:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Akawaamuru wale waliomshitaki waje kwako.] Wewe mwenyewe kwa kumwulizauliza utaweza kupata habari ya mambo yale yote tunayomshitaki sisi.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kisha akaamuru washtaki wake waje mbele yako.] Kama ukimhoji wewe mwenyewe, utaweza kubainisha mambo haya yote tunayomshtaki kwayo.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kisha akaamuru washtaki wake waje mbele yako.] Kama ukimhoji wewe mwenyewe, utaweza kubainisha mambo haya yote tunayomshtaki kwayo.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kama ukimhoji wewe mwenyewe, utaweza kubainisha mambo haya yote tunayomshtaki kwayo.”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

akiwaamuru washtaki wake waje mbele yako.] Kwa kumchunguza mwenyewe utaweza kujua ukweli kuhusu mashtaka haya yote tunayoleta dhidi yake.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

akiwaamuru washtaki wake waje mbele yako: ili] kwa kumchunguza wewe mwenyewe unaweza kujua kutoka kwake mambo yote tunayomshtaki kwayo.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Akawaamuru wale waliomshitaki waje kwako.] Wewe mwenyewe kwa kumwulizauliza utaweza kupata habari ya mambo yale yote tunayomshitaki sisi.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Matendo 24:8
7 Marejeleo ya Msalaba  

akawaambia, Mtu huyu mmemleta kwangu kana kwamba anapotosha watu; nami, tazama, nimeamua mambo yake mbele yenu, ila sikuona kwake kosa lolote katika mambo hayo mliyomshitaki;


Hata nilipopewa habari kwamba patakuwa na ghasia juu ya mtu huyu, mara nikamtuma kwako, nikawaagiza na wale waliomshitaki, wanene habari zake mbele yako. Wasalamu.


akasema, Nitakusikia wewe watakapokuja wale waliokushitaki; akaamuru alindwe katika nyumba ya utawala wa Herode.


Lakini Lisia jemadari akafika akamwondoa mikononi mwetu kwa nguvu,


Wayahudi nao wakamshitaki, wakisema ya kuwa ndivyo yalivyo.


Akasema, Wale walio na mamlaka kwenu na wateremke pamoja nami wakamshitaki, ikiwa liko neno baya katika mtu huyu.