Bali mimi nawaambieni, Kila amkasirikiaye ndugu yake itampasa hukumu; na mtu akimtusi ndugu yake, anastahili kuhukumiwa na baraza; na mtu akimwambia nduguye, Ewe mpumbavu, anastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.
Matendo 23:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nami nikitaka kulijua lile neno walilomshitakia, nikamteremsha nikamweka mbele ya baraza; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nilimpeleka mbele ya Baraza lao kuu nikitaka kujua kisa cha mashtaka yao. Biblia Habari Njema - BHND Nilimpeleka mbele ya Baraza lao kuu nikitaka kujua kisa cha mashtaka yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nilimpeleka mbele ya Baraza lao kuu nikitaka kujua kisa cha mashtaka yao. Neno: Bibilia Takatifu Nilitaka kujua kwa nini walikuwa wanamshutumu, hivyo nikamleta mbele ya Baraza la Wayahudi. Neno: Maandiko Matakatifu Nilitaka kujua kwa nini walikuwa wanamshutumu, hivyo nikamleta mbele ya baraza lao. BIBLIA KISWAHILI Nami nikitaka kulijua lile neno walilomshitakia, nikamteremsha nikamweka mbele ya baraza; |
Bali mimi nawaambieni, Kila amkasirikiaye ndugu yake itampasa hukumu; na mtu akimtusi ndugu yake, anastahili kuhukumiwa na baraza; na mtu akimwambia nduguye, Ewe mpumbavu, anastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.
Kesho yake akitaka kujua hakika, ni kwa sababu gani ameshitakiwa na Wayahudi, akamfungua, akawaamuru wakuu wa makuhani na baraza yote wakutane. Akamleta Paulo chini, akamweka mbele yao.
Paulo akawakazia macho watu wa baraza, akasema, Ndugu zangu, mimi kwa dhamiri safi kabisa nimeishi mbele za Mungu hata leo hivi.
Ugomvi mkubwa ulipotokea, yule jemadari akahofia Paulo asije akararuliwa nao, akaamuru askari washuke na kumwondoa kwa nguvu mikononi mwao, na kumleta ndani ya ngome.