nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu,
Matendo 23:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Klaudio Lisia kwa mtawala mtukufu Feliki, Salamu! Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mimi Klaudio Lusia ninakuandikia wewe Mheshimiwa Felisi, mkuu wa mkoa. Salamu! Biblia Habari Njema - BHND “Mimi Klaudio Lusia ninakuandikia wewe Mheshimiwa Felisi, mkuu wa mkoa. Salamu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mimi Klaudio Lusia ninakuandikia wewe Mheshimiwa Felisi, mkuu wa mkoa. Salamu! Neno: Bibilia Takatifu Klaudio Lisia. Kwa Mtawala, Mtukufu Feliksi. Salamu. Neno: Maandiko Matakatifu Klaudio Lisia, Kwa Mtawala, Mtukufu Feliksi: Salamu. BIBLIA KISWAHILI Klaudio Lisia kwa mtawala mtukufu Feliki, Salamu! |
nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu,
Mitume na ndugu wazee, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shamu na Kilikia, walio wa Mataifa; Salamu.
Akawaambia kuweka wanyama tayari wampandishe Paulo, na kumchukua salama kwa Feliki mtawala.
Lakini Paulo akasema, Sina wazimu, Ee Festo mtukufu, bali nanena maneno ya kweli na ya akili kamili.
Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo, kwa makabila kumi na mawili waliotawanyika; salamu.