Matendo 22:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa maana utakuwa shahidi wake kwa watu wote, wa mambo hayo uliyoyaona na kuyasikia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa maana utamshuhudia kwa watu wote ukiwaambia yale uliyoyaona na kuyasikia. Biblia Habari Njema - BHND Kwa maana utamshuhudia kwa watu wote ukiwaambia yale uliyoyaona na kuyasikia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa maana utamshuhudia kwa watu wote ukiwaambia yale uliyoyaona na kuyasikia. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa utakuwa shahidi wake kwa watu kuhusu kile ulichokiona na kukisikia. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa utakuwa shahidi wake kwa watu kuhusu kile ulichokiona na kukisikia. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana utakuwa shahidi wake kwa watu wote, wa mambo hayo uliyoyaona na kuyasikia. |
kuanza tangu ubatizo wa Yohana, hata siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi.
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na kote katika Yudea, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Akasema, Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe upate kujua mapenzi yake, na kumwona yule Mwenye haki, na kuisikia sauti itokayo katika kinywa chake.
Usiku ule Bwana akasimama karibu naye, akasema, Uwe na moyo mkuu; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia habari zangu Yerusalemu, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi nako.
bali kwanza niliwahubiria wale wa Dameski na Yerusalemu, na katika nchi yote ya Yudea, na watu wa Mataifa, kwamba watubu na kumwelekea Mungu, wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao.
akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe.