na alipokwisha kushuka Kaisaria, akapanda juu, akawasalimu kanisa, kisha akateremka kwenda Antiokia.
Matendo 21:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Baada ya siku zile tukachukua vyombo vyetu tukapanda kwenda Yerusalemu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya kukaa pale kwa muda, tulifunga mizigo yetu, tukaendelea na safari kwenda Yerusalemu. Biblia Habari Njema - BHND Baada ya kukaa pale kwa muda, tulifunga mizigo yetu, tukaendelea na safari kwenda Yerusalemu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya kukaa pale kwa muda, tulifunga mizigo yetu, tukaendelea na safari kwenda Yerusalemu. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya haya, tukajiandaa, tukaondoka kwenda Yerusalemu. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya haya, tukajiandaa, tukaondoka kwenda Yerusalemu. BIBLIA KISWAHILI Baada ya siku zile tukachukua vyombo vyetu tukapanda kwenda Yerusalemu. |
na alipokwisha kushuka Kaisaria, akapanda juu, akawasalimu kanisa, kisha akateremka kwenda Antiokia.
Mambo hayo yalipokwisha kumalizika, Paulo akaazimu rohoni mwake, akiisha kupita katika Makedonia na Akaya, aende Yerusalemu, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi pia.
Basi tuliposikia haya, sisi na watu wa mahali pale, tukamsihi asipande kwenda Yerusalemu.
Festo alipokwisha kuingia katika mkoa, baada ya siku tatu akapanda kwenda Yerusalemu kutoka Kaisaria.
Alipokwisha kukaa kwao siku nane au kumi si zaidi, akateremkia Kaisaria; na siku ya pili akaketi katika kiti cha hukumu akaamuru Paulo aletwe.
Lakini Festo akitaka kujipendekeza kwa Wayahudi akamjibu Paulo, akisema, Je! Wataka kwenda Yerusalemu, ukahukumiwe huko mbele yangu kwa ajili ya mambo hayo?