Mungu Mwenyezi na awape rehema usoni pa mtu yule ili awafungulie ndugu yenu huyo mwingine, na Benyamini. Nami nikifiwa na watoto wangu, nimefiwa.
Matendo 21:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Alipokataa shauri letu, tukanyamaza tukisema, Mapenzi ya Bwana na yatendeke. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tuliposhindwa kumshawishi tulinyamaza, tukasema tu: “Atakalo Bwana lifanyike!” Biblia Habari Njema - BHND Tuliposhindwa kumshawishi tulinyamaza, tukasema tu: “Atakalo Bwana lifanyike!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tuliposhindwa kumshawishi tulinyamaza, tukasema tu: “Atakalo Bwana lifanyike!” Neno: Bibilia Takatifu Alipokataa kushawishika, tukaacha kumsihi, tukasema, “Mapenzi ya Mwenyezi Mungu na yatendeke.” Neno: Maandiko Matakatifu Alipokuwa hashawishiki, tukaacha kumsihi, tukasema, “Mapenzi ya Mwenyezi Mungu na yatendeke.” BIBLIA KISWAHILI Alipokataa shauri letu, tukanyamaza tukisema, Mapenzi ya Bwana na yatendeke. |
Mungu Mwenyezi na awape rehema usoni pa mtu yule ili awafungulie ndugu yenu huyo mwingine, na Benyamini. Nami nikifiwa na watoto wangu, nimefiwa.
Ndipo Hezekia akamwambia Isaya, Neno la BWANA ulilolinena ni jema. Tena akasema, Je! Sivyo, ikiwapo amani na kweli katika siku zangu?
Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniondokee; lakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.
Akaenda tena mara ya pili, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniondokee nisipokunywa, mapenzi yako yatimizwe.
Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.]
akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; lakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. [
Basi Samweli akamwambia kila neno, asimfiche lolote. Naye akasema, Ndiye BWANA; na afanye alionalo kuwa ni jema.