Musa akakasirika sana, akamwambia BWANA. Usiikubali sadaka yao; mimi sikutwaa hata punda mmoja kwao, wala sikumwumiza hata mtu mmoja miongoni mwao.
Matendo 20:33 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mimi sikutamani hata mara moja fedha, wala dhahabu, wala nguo za mtu yeyote. Biblia Habari Njema - BHND Mimi sikutamani hata mara moja fedha, wala dhahabu, wala nguo za mtu yeyote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mimi sikutamani hata mara moja fedha, wala dhahabu, wala nguo za mtu yeyote. Neno: Bibilia Takatifu Sikutamani fedha wala dhahabu wala vazi la mtu yeyote. Neno: Maandiko Matakatifu Sikutamani fedha wala dhahabu wala vazi la mtu yeyote. BIBLIA KISWAHILI Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu. |
Musa akakasirika sana, akamwambia BWANA. Usiikubali sadaka yao; mimi sikutwaa hata punda mmoja kwao, wala sikumwumiza hata mtu mmoja miongoni mwao.
Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo.
Lakini mimi sikutumia mambo hayo hata moja. Wala siyaandiki hayo ili iwe hivyo kwangu mimi; maana ni heri nife kuliko mtu awaye yote abatilishe huku kujisifu kwangu.
Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa ninapohubiri, nitaitoa Injili bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili.
Je! Nilifanya dhambi kwa kunyenyekea ili ninyi mtukuzwe, kwa sababu niliwahubiria Injili ya Mungu bila ujira?
Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote najilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena najilinda.
Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu yeyote, wala kumharibu mtu, wala kumkosea mtu.
Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wowote, kama mjuavyo, wala maneno ya juu juu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi.
lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.