Matendo 20:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Toka Mileto Paulo akatuma watu kwenda Efeso, akawaita wazee wa kanisa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kutoka Mileto Paulo alituma ujumbe kwa wazee wa Efeso wakutane naye. Biblia Habari Njema - BHND Kutoka Mileto Paulo alituma ujumbe kwa wazee wa Efeso wakutane naye. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kutoka Mileto Paulo alituma ujumbe kwa wazee wa Efeso wakutane naye. Neno: Bibilia Takatifu Paulo akiwa Mileto, alituma mjumbe kwenda Efeso kuwaita wazee wa kundi la waumini waje wakutane naye. Neno: Maandiko Matakatifu Paulo akiwa Mileto, alituma mjumbe kwenda Efeso kuwaita wazee wa kundi la waumini waje wakutane naye. BIBLIA KISWAHILI Toka Mileto Paulo akatuma watu kwenda Efeso, akawaita wazee wa kanisa. |
Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.
Mitume na ndugu wazee, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shamu na Kilikia, walio wa Mataifa; Salamu.
Walipofika Yerusalemu wakakaribishwa na kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao.
Basi walipokuwa wakipita kati ya miji ile, wakawapa zile amri zilizoamriwa na mitume na wazee walioko Yerusalemu, ili wazishike.
Wakafika Efeso, akawaacha huko. Yeye mwenyewe akaingia katika sinagogi, akahojiana na Wayahudi.
Tukatweka kutoka huko, na siku ya pili tukafika mahali panapokabili Kio; siku ya tatu tukawasili Samo, tukakaa Trogilio, siku ya nne tukafika Mileto.
Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kutoa unabii na kufundisha.
Kwa sababu hii nilikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuwateua wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru;
Mtu wa kwenu amekuwa mgonjwa? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.
Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye;
Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuayo ile kweli;