Ametoa kwa ukarimu, na kuwapa maskini, Haki yake yakaa milele, Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.
Matendo 2:45 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kulingana na haja ya kila mmoja. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walikuwa wakiuza mali na vitu vyao kisha wakagawana fedha kadiri ya mahitaji ya kila mmoja. Biblia Habari Njema - BHND Walikuwa wakiuza mali na vitu vyao kisha wakagawana fedha kadiri ya mahitaji ya kila mmoja. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walikuwa wakiuza mali na vitu vyao kisha wakagawana fedha kadiri ya mahitaji ya kila mmoja. Neno: Bibilia Takatifu Waliuza mali yao na vitu walivyokuwa navyo, kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake. Neno: Maandiko Matakatifu Waliuza mali zao na vitu walivyokuwa navyo, kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake. BIBLIA KISWAHILI wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kulingana na haja ya kila mmoja. |
Ametoa kwa ukarimu, na kuwapa maskini, Haki yake yakaa milele, Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.
Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, nenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
Nami nawaambia, Jifanyieni rafiki kwa mali ya duniani, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele.
Yesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha, njoo unifuate.
Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne.
Na wale wanafunzi, kila mtu kwa kadiri ya alivyofanikiwa, wakaazimu kupeleka msaada kwa ndugu zao waliokaa Yudea.
Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa,
Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?