Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako kuna furaha tele; Na katika mkono wako wa kulia Mna mema ya milele.
Matendo 2:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Umenijulisha njia za uzima; Utanijaza furaha kwa uso wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Umenionesha njia za uhai, umenijaza furaha kwa kuwako kwako!’ Biblia Habari Njema - BHND Umenionesha njia za uhai, umenijaza furaha kwa kuwako kwako!’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Umenionesha njia za uhai, umenijaza furaha kwa kuwako kwako!’ Neno: Bibilia Takatifu Umenionesha njia za uzima, utanijaza na furaha mbele zako.’ Neno: Maandiko Matakatifu Umenionyesha njia za uzima, utanijaza na furaha mbele zako.’ BIBLIA KISWAHILI Umenijulisha njia za uzima; Utanijaza furaha kwa uso wako. |
Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako kuna furaha tele; Na katika mkono wako wa kulia Mna mema ya milele.
Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumainie Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.
Wanaume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo.
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.