Lakini Abishai, mwana wa Seruya, akamsaidia, akampiga Mfilisti, akamwua. Ndipo watu wa Daudi wakamwapia, wakasema, Wewe hutatoka tena pamoja nasi kwenda vitani, usije ukaizima taa ya Israeli.
Matendo 19:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na Paulo alipotaka kuingia kati ya watu, wanafunzi hawakumwacha aingie. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Paulo mwenyewe alitaka kuukabili huo umati wa watu, lakini wale waumini walimzuia. Biblia Habari Njema - BHND Paulo mwenyewe alitaka kuukabili huo umati wa watu, lakini wale waumini walimzuia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Paulo mwenyewe alitaka kuukabili huo umati wa watu, lakini wale waumini walimzuia. Neno: Bibilia Takatifu Paulo akataka kuingia katikati ya umati, lakini wanafunzi hawakumruhusu. Neno: Maandiko Matakatifu Paulo akataka kuingia katikati ya umati huo, lakini wanafunzi hawakumruhusu. BIBLIA KISWAHILI Na Paulo alipotaka kuingia kati ya watu, wanafunzi hawakumwacha aingie. |
Lakini Abishai, mwana wa Seruya, akamsaidia, akampiga Mfilisti, akamwua. Ndipo watu wa Daudi wakamwapia, wakasema, Wewe hutatoka tena pamoja nasi kwenda vitani, usije ukaizima taa ya Israeli.
Na baadhi ya wakuu wa Asia, walio rafiki zake, wakatuma watu kwake, wakimsihi asiingie ndani katika ukumbi wa michezo.
Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; basi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi, akahojiana na watu kila siku katika darasa la mtu mmoja, jina lake Tirano.
Paulo akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, mtu wa Tarso, mji wa Kilikia, mwenyeji wa mji usiokuwa mnyonge. Nakuomba, nipe ruhusa niseme na wenyeji hawa.