ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
Matendo 19:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hivyo ndivyo neno la Bwana lilivyozidi na kushinda kwa nguvu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa namna hiyo, neno la Bwana lilizidi kuenea na kuwa na nguvu zaidi. Biblia Habari Njema - BHND Kwa namna hiyo, neno la Bwana lilizidi kuenea na kuwa na nguvu zaidi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa namna hiyo, neno la Bwana lilizidi kuenea na kuwa na nguvu zaidi. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo neno la Bwana Isa likaenea sana na kuwa na nguvu. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo neno la Bwana Isa likaenea sana na kuwa na nguvu. BIBLIA KISWAHILI Hivyo ndivyo neno la Bwana lilivyozidi na kushinda kwa nguvu. |
ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
Ndipo yule mtawala, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.
Mambo haya yakaendelea kwa muda wa miaka miwili, hata wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wagiriki.
Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.
Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa kote kama ilivyo kwenu;