Kwa maana nimemchagua ili awaamuru wanawe na vizazi vyake baada yake wadumishe njia ya BWANA, kwa kuwa wenye haki na kweli, ili BWANA naye akamtimizie Abrahamu ahadi zake.
Matendo 18:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa bidii habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alikuwa amefundishwa juu ya hiyo njia ya Bwana, na akiwa motomoto, aliongea juu ya habari za Yesu akafundisha kwa usahihi ingawa alikuwa amepata ubatizo wa Yohane tu. Biblia Habari Njema - BHND Alikuwa amefundishwa juu ya hiyo njia ya Bwana, na akiwa motomoto, aliongea juu ya habari za Yesu akafundisha kwa usahihi ingawa alikuwa amepata ubatizo wa Yohane tu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alikuwa amefundishwa juu ya hiyo njia ya Bwana, na akiwa motomoto, aliongea juu ya habari za Yesu akafundisha kwa usahihi ingawa alikuwa amepata ubatizo wa Yohane tu. Neno: Bibilia Takatifu Alikuwa amefundishwa katika njia ya Bwana Isa, naye alikuwa na bidii katika roho, akafundisha kwa usahihi kuhusu Isa, ingawa alijua tu ubatizo wa Yahya. Neno: Maandiko Matakatifu Alikuwa amefundishwa katika njia ya Bwana Isa, naye alikuwa na bidii katika roho, akafundisha kwa usahihi juu ya Isa, ingawa alijua tu ubatizo wa Yahya. BIBLIA KISWAHILI Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa bidii habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu. |
Kwa maana nimemchagua ili awaamuru wanawe na vizazi vyake baada yake wadumishe njia ya BWANA, kwa kuwa wenye haki na kweli, ili BWANA naye akamtimizie Abrahamu ahadi zake.
Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya BWANA; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.
BWANA asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, Iko wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo.
Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za BWANA zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake.
Hata walipofika walimwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu; lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! Ni halali kumpa Kaisari kodi au siyo?
Na watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana.
akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyooka?
Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu.
Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Priskila na Akila walipomsikia wakampeleka kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.
Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; basi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi, akahojiana na watu kila siku katika darasa la mtu mmoja, jina lake Tirano.
akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, wanaume kwa wanawake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
Askari aliye vitani hajiingizi katika shughuli za dunia, maana lengo lake ni kumpendeza yeye aliyemweka kuwa askari.
Basi ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, ili mpate kuponywa. Sala yake mwenye haki ina nguvu nyingi, na hutenda mengi.
ili kwa njia ya hayo nipate kuwajaribu Israeli, kama wataifuata njia ya BWANA kwenda katika njia hiyo, au sivyo.
Lakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka