Lakini watakapowafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawaambia, Hamtaimaliza miji ya Israeli, hata ajapo Mwana wa Adamu.
Matendo 17:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mara hiyo wale ndugu wakamtuma Paulo aende zake mpaka pwani; bali Sila na Timotheo wakabakia huko. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wale ndugu wakamsindikiza haraka aende pwani lakini Sila na Timotheo walibaki Berea. Biblia Habari Njema - BHND Wale ndugu wakamsindikiza haraka aende pwani lakini Sila na Timotheo walibaki Berea. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wale ndugu wakamsindikiza haraka aende pwani lakini Sila na Timotheo walibaki Berea. Neno: Bibilia Takatifu Mara hiyo, wale ndugu wakamsafirisha Paulo hadi pwani, lakini Sila na Timotheo wakabaki Beroya. Neno: Maandiko Matakatifu Mara hiyo, wale ndugu wakamsafirisha Paulo hadi pwani, lakini Sila na Timotheo wakabaki Beroya. BIBLIA KISWAHILI Mara hiyo wale ndugu wakamtuma Paulo aende zake mpaka pwani; bali Sila na Timotheo wakabakia huko. |
Lakini watakapowafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawaambia, Hamtaimaliza miji ya Israeli, hata ajapo Mwana wa Adamu.
Siku zile akasimama Petro kati ya hao ndugu (jumla ya majina ilikuwa mia moja na ishirini), akasema,
Basi ikawapendeza mitume na wazee na kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwatuma Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba; nao ni hawa, Yuda aliyeitwa Barsaba, na Sila, waliokuwa watu wakuu katika ndugu. Wakaandika hivi na kupeleka kwa mikono yao,
Basi akafika Derbe na Listra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke Myahudi aliyeamini; lakini babaye alikuwa Mgiriki.
Mara hao ndugu wakawatuma Paulo na Sila usiku hadi Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi.
Lakini wale waliomsindikiza Paulo wakampeleka mpaka Athene; nao wakiisha kupokea maagizo kuwapelekea Sila na Timotheo, ya kwamba wasikawie kumfuata, wakaenda zao.
Wengine miongoni mwao wakaamini, wakafuatana na Paulo na Sila; na Wagiriki waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache.
na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako,
Hata Sila na Timotheo walipoteremka kutoka Makedonia, Paulo akasongwa sana na lile neno, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo.
Akatuma watu wawili miongoni mwa wale waliomtumikia kwenda Makedonia, nao ni Timotheo na Erasto, yeye mwenyewe akakaa katika Asia kwa muda.
Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, na Wayahudi kumfanyia vitimvi, alipotaka kwenda Shamu kwa njia ya bahari; basi akaazimu kurejea kwa njia ya Makedonia.
Kama vile nilivyokusihi ukae Efeso, nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, ili uwakataze wengine wasifundishe elimu nyingine;
Kwa sababu hii nilikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuwateua wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru;
Akawaambia, Nendeni zenu mlimani, wale wanaowafuatia wasije wakawapata; mkajifiche huko siku tatu hadi wao wanaowafuatia watakaporudi; kisha nendeni zenu.