Matendo 16:36 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yule mlinzi wa gereza akamwarifu Paulo maneno haya akisema, Mahakimu wametuma watu ili mfunguliwe; basi, sasa tokeni nje, nendeni zenu kwa amani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yule askari wa gereza alimpasha habari Paulo: “Mahakimu wametuma ujumbe ili mfunguliwe. Sasa mnaweza kutoka na kwenda zenu kwa amani.” Biblia Habari Njema - BHND Yule askari wa gereza alimpasha habari Paulo: “Mahakimu wametuma ujumbe ili mfunguliwe. Sasa mnaweza kutoka na kwenda zenu kwa amani.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yule askari wa gereza alimpasha habari Paulo: “Mahakimu wametuma ujumbe ili mfunguliwe. Sasa mnaweza kutoka na kwenda zenu kwa amani.” Neno: Bibilia Takatifu Mkuu wa gereza akamwambia Paulo “Mahakimu wameagiza niwaachie huru, kwa hiyo tokeni na mwende zenu kwa amani.” Neno: Maandiko Matakatifu Mkuu wa gereza akamwambia Paulo “Mahakimu wameagiza niwaache huru, kwa hiyo tokeni na mwende zenu kwa amani.” BIBLIA KISWAHILI Yule mlinzi wa gereza akamwarifu Paulo maneno haya akisema, Mahakimu wametuma watu ili mfunguliwe; basi, sasa tokeni nje, nendeni zenu kwa amani. |
Basi Musa akaenda na kurejea kwa Yethro mkwewe, na kumwambia, Nipe ruhusa niende, nakusihi, niwarudie hao ndugu zangu walioko Misri, nipate kuwaona kwamba wako hai hata sasa. Yethro akamwambia Musa, Haya, nenda kwa amani.
Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, nenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.
Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.
Na wakiisha kukaa huko muda, wakaruhusiwa na ndugu waende kwa amani kwa hao waliowatuma. [
Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana.
Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia.
Kulipopambazuka mahakimu wakawatuma wakubwa wa askari wakisema, Waacheni watu wale waende zao.
Ndipo Eli akajibu, akasema, Nenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.
Naye Yonathani akamwambia Daudi, Nenda kwa amani; kwa maana sisi sote wawili tumeapiana kwa jina la BWANA ya kwamba, BWANA atakuwa kati ya mimi na wewe, na kati ya uzao wangu na uzao wako milele. Daudi akaondoka, akaenda zake; Yonathani naye akaenda zake mjini.
Basi Daudi akapokea mkononi mwake vitu vile alivyomletea; akamwambia, Haya! Kwea kwa amani kwenda nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako, nami nimelikubali ombi lako.