Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda katika mashua, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani.
Matendo 16:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tulidhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku ya Sabato tulitoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto ambapo tulidhani ya kuwa ni mahali pa kusali. Tuliketi, tukaongea na wanawake waliokusanyika mahali hapo. Biblia Habari Njema - BHND Siku ya Sabato tulitoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto ambapo tulidhani ya kuwa ni mahali pa kusali. Tuliketi, tukaongea na wanawake waliokusanyika mahali hapo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku ya Sabato tulitoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto ambapo tulidhani ya kuwa ni mahali pa kusali. Tuliketi, tukaongea na wanawake waliokusanyika mahali hapo. Neno: Bibilia Takatifu Siku ya Sabato tukaenda nje ya lango la mji kando ya mto, ambapo tulitarajia kupata mahali pa kufanyia maombi. Tukaketi, tukaanza kuongea na baadhi ya wanawake waliokuwa wamekusanyika huko. Neno: Maandiko Matakatifu Siku ya Sabato tukaenda nje ya lango la mji kando ya mto, mahali ambapo tulitarajia tungepata mahali pa kufanyia maombi. Tukaketi, tukaanza kuongea na baadhi ya wanawake waliokuwa wamekusanyika huko. BIBLIA KISWAHILI Siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tulidhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale. |
Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda katika mashua, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani.
Asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha.
Lakini wao wakatoka Perge, wakapita kati ya nchi, wakafika Antiokia, mji wa Pisidia, wakaingia katika sinagogi siku ya sabato, wakaketi.
Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, tulikutana na kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi, aliyewapatia bwana zake faida kubwa kwa kuagua.
Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia.
Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimokuwa, akahojiana nao kwa maneno ya Maandiko sabato tatu,
Siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubia, maana aliazimia kusafiri siku iliyofuata, naye akafululiza maneno yake hadi usiku wa manane.
Hata tulipotimiza siku zile tukaondoka tukaenda zetu, na watu wote, pamoja na wake zao na watoto wao, wakatusindikiza mpake nje ya mji, tukapiga magoti pwani tukaomba;
Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu.
mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa kwa viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nilikuwa mhudumu wake.