Matendo 15:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hakufanya ubaguzi wowote kati yetu na wao; aliitakasa mioyo yao kwa imani. Biblia Habari Njema - BHND Hakufanya ubaguzi wowote kati yetu na wao; aliitakasa mioyo yao kwa imani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hakufanya ubaguzi wowote kati yetu na wao; aliitakasa mioyo yao kwa imani. Neno: Bibilia Takatifu Mungu hakutofautisha kati yetu na wao, bali alitakasa mioyo yao kwa imani. Neno: Maandiko Matakatifu Mungu hakutofautisha kati yetu na wao, bali alitakasa mioyo yao kwa imani. BIBLIA KISWAHILI wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani. |
Tena itakuwa mtaigawanya kwa kura, kuwa urithi kwenu, na kwa wageni wakaao kwenu kama ugeni, watakaozaa watoto kati yenu, nao watakuwa kwenu, kama wazaliwa miongoni mwa wana wa Israeli; watakuwa na urithi pamoja nanyi kati ya makabila ya Israeli.
Akawaambia, Ninyi mnajua ya kuwa si halali kwa mtu aliye Myahudi ashirikiane na mtu wa taifa lingine wala kumtembelea, lakini Mungu amenionya, nisimwite mtu yeyote mchafu wala najisi.
Roho akaniambia nifuatane nao, nisione tashwishi. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule;
Ikawa huko Ikonio wakaingia pamoja katika sinagogi la Wayahudi; na kwa vile walivyonena, kundi kubwa la Wayahudi na la Wagiriki wakaamini.
Hata walipofika wakalikutanisha kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwamba amewafungulia Mataifa mlango wa imani.
ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;
Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La! Hata kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wagiriki ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi;
kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu.
Je! Mtu fulani ameitwa akiwa amekwisha kutahiriwa? Asijifanye kana kwamba hakutahiriwa. Mtu fulani ameitwa akiwa hajatahiriwa bado? Basi asitahiriwe.
Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu.
Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutotahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili;
Hapo hapana Mgiriki wala Myahudi, kutahiriwa wala kutotahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala muungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote.
Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo safi.