Na alipokuwa akifikiri haya akafika nyumbani kwa Mariamu, mamaye Yohana, ambaye jina lake la pili ni Marko; na watu wengi walikuwa wamekutana humo wakiomba.
Matendo 15:37 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyeitwa Marko pamoja nao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Barnaba alitaka wamchukue pia Yohane aitwaye Marko. Biblia Habari Njema - BHND Barnaba alitaka wamchukue pia Yohane aitwaye Marko. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Barnaba alitaka wamchukue pia Yohane aitwaye Marko. Neno: Bibilia Takatifu Barnaba alitaka wamchukue Yohana aitwaye Marko waende naye. Neno: Maandiko Matakatifu Barnaba alitaka wamchukue Yohana aitwaye Marko waende naye. BIBLIA KISWAHILI Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyeitwa Marko pamoja nao. |
Na alipokuwa akifikiri haya akafika nyumbani kwa Mariamu, mamaye Yohana, ambaye jina lake la pili ni Marko; na watu wengi walikuwa wamekutana humo wakiomba.
Na Barnaba na Sauli, walipokwisha kutimiza huduma yao, wakarejea kutoka Yerusalemu, wakamchukua pamoja nao Yohana aitwaye Marko.
Kisha Paulo na wenziwe wakang'oa nanga wakasafiri kutoka Pafo, wakafika Perge katika Pamfilia. Yohana akawaacha akarejea Yerusalemu.
Na walipokuwa katika Salami wakalihubiri neno la Mungu katika masinagogi ya Wayahudi, nao walikuwa naye Yohana kuwa mtumishi wao.
Basi palitokea mashindano baina yao hata wakatengana. Barnaba akamchukua Marko akaabiri kwenda Kipro.
Aristarko, aliyefungwa pamoja nami, awasalimu; pamoja na Marko, binamu yake Barnaba, ambaye mmepokea maagizo juu yake; akifika kwenu mkaribisheni.
Luka peke yake yupo hapa pamoja nami. Umtwae Marko, umlete pamoja nawe, maana anifaa kwa utumishi.