Matendo 15:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Isiwe hivyo, ila tunaamini kwamba, sisi kama vile wao, tutaokolewa kwa njia ya neema ya Bwana Yesu.” Biblia Habari Njema - BHND Isiwe hivyo, ila tunaamini kwamba, sisi kama vile wao, tutaokolewa kwa njia ya neema ya Bwana Yesu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Isiwe hivyo, ila tunaamini kwamba, sisi kama vile wao, tutaokolewa kwa njia ya neema ya Bwana Yesu.” Neno: Bibilia Takatifu Lakini sisi tunaamini ya kuwa tunaokolewa kwa neema ya Bwana wetu Isa Al-Masihi, kama wao wanavyookolewa.” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini sisi tunaamini ya kuwa tunaokolewa kwa neema ya Bwana Isa Al-Masihi, kama wao wanavyookolewa.” BIBLIA KISWAHILI Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao. |
Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
Nashangaa kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia Injili ya namna nyingine.
Lakini tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki.
Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuifungua mihuri yake; kwa kuwa ulichinjwa, ukawa fidia kwa Mungu na kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,