Matendo 13:49 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Neno la Bwana likaenea kila mahali katika sehemu ile. Biblia Habari Njema - BHND Neno la Bwana likaenea kila mahali katika sehemu ile. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Neno la Bwana likaenea kila mahali katika sehemu ile. Neno: Bibilia Takatifu Neno la Bwana likaenea katika eneo lile lote. Neno: Maandiko Matakatifu Neno la Bwana Isa likaenea katika eneo lile lote. BIBLIA KISWAHILI Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote. |
Ndipo yule mtawala, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.
Mambo haya yakaendelea kwa muda wa miaka miwili, hata wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wagiriki.
Tena mnaona na kusikia ya kwamba si katika Efeso tu, bali katika Asia yote pia Paulo huyo ameshawishi watu wengi na kuwageuza nia zao, akisema ya kwamba hiyo inayofanywa kwa mikono siyo miungu.
Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.