Matendo 12:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Neno la Bwana likazidi na kuenea. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Neno la Mungu likazidi kuenea na kukua. Biblia Habari Njema - BHND Neno la Mungu likazidi kuenea na kukua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Neno la Mungu likazidi kuenea na kukua. Neno: Bibilia Takatifu Lakini neno la Mungu likaendelea mbele na kuenea, nao wengi wakaambatana nalo. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini neno la Mwenyezi Mungu likaendelea mbele na kuenea, nao wengi wakaambatana nalo. BIBLIA KISWAHILI Neno la Bwana likazidi na kuenea. |
Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;
Basi Danieli akaenda kwa Arioko, aliyewekwa na mfalme kuwaangamiza wenye hekima wa Babeli; alikwenda akamwambia hivi, Usiwaangamize wenye hekima wa Babeli; niingize mimi mbele ya mfalme, nami nitamwonesha mfalme ile tafsiri.
Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu.
Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.
iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, na kuzaa matunda na kukua, kama inavyokua kwenu pia, tangu siku mlipoisikia mkaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli;
Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa kote kama ilivyo kwenu;