Matendo 10:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na katika kusema naye akaingia ndani, akaona watu wengi wamekusanyika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Petro aliendelea kuongea na Kornelio wakiwa wanaingia nyumbani ambamo aliwakuta watu wengi wamekusanyika. Biblia Habari Njema - BHND Petro aliendelea kuongea na Kornelio wakiwa wanaingia nyumbani ambamo aliwakuta watu wengi wamekusanyika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Petro aliendelea kuongea na Kornelio wakiwa wanaingia nyumbani ambamo aliwakuta watu wengi wamekusanyika. Neno: Bibilia Takatifu Petro alipokuwa akizungumza naye, akaingia ndani na kuwakuta watu wengi wamekusanyika. Neno: Maandiko Matakatifu Petro alipokuwa akizungumza naye akaingia ndani na kukuta watu wengi wamekusanyika. BIBLIA KISWAHILI Na katika kusema naye akaingia ndani, akaona watu wengi wamekusanyika. |
Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yanakuja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno.
Kesho yake wakaingia Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwangojea, akiwa amekusanya jamaa zake na rafiki zake.
Hata walipofika wakalikutanisha kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwamba amewafungulia Mataifa mlango wa imani.
mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,