Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake.
Matendo 10:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi inuka ushuke ufuatane nao, usione tashwishi, kwa maana ni mimi niliyewatuma. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Shuka upesi na wala usisite kwenda pamoja nao kwa maana ni mimi niliyewatuma.” Biblia Habari Njema - BHND Shuka upesi na wala usisite kwenda pamoja nao kwa maana ni mimi niliyewatuma.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Shuka upesi na wala usisite kwenda pamoja nao kwa maana ni mimi niliyewatuma.” Neno: Bibilia Takatifu Inuka na ushuke, usisite kwenda nao kwa kuwa mimi nimewatuma.” Neno: Maandiko Matakatifu Inuka na ushuke, usisite kwenda nao kwa kuwa mimi nimewatuma.” BIBLIA KISWAHILI Basi inuka ushuke ufuatane nao, usione tashwishi, kwa maana ni mimi niliyewatuma. |
Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake.
Roho akaniambia nifuatane nao, nisione tashwishi. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule;
Basi watu hao, walipotumwa hadi Kipro na Roho Mtakatifu wakateremkia Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hata Kipro.
Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile iteremkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa.
Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.
Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.
Ila na aombe kwa imani, pasipo mashaka yoyote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari linalochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.