Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi.
Matendo 10:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Jambo hili likatendeka mara tatu; kisha kile chombo kikapokewa tena mbinguni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Jambo hili lilifanyika mara tatu, kisha ile shuka ikarudishwa juu mbinguni. Biblia Habari Njema - BHND Jambo hili lilifanyika mara tatu, kisha ile shuka ikarudishwa juu mbinguni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Jambo hili lilifanyika mara tatu, kisha ile shuka ikarudishwa juu mbinguni. Neno: Bibilia Takatifu Jambo hili lilitokea mara tatu, na ghafula kile kitambaa kikarudishwa mbinguni. Neno: Maandiko Matakatifu Jambo hili lilitokea mara tatu na ghafula ile nguo ikarudishwa mbinguni. BIBLIA KISWAHILI Jambo hili likatendeka mara tatu; kisha kile chombo kikapokewa tena mbinguni. |
Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi.
Na roho hiyo ikaniinua, ikanichukua katika maono, kwa nguvu za Roho ya Mungu, hadi Ukaldayo, kwa watu wale wa uhamisho. Basi maono niliyoyaona yakaniacha.
Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.
Wakati Petro alipokuwa akisumbuka ndani ya nafsi yake, juu ya maana ya maono hayo aliyoyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, wakatokeza. Walikuwa kukiulizia nyumba ya Simoni, wakiwa wamesimama mbele ya lango,
Hii ndiyo mara yangu ya tatu kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.