Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo, Moyo wake hujikusanyia maovu, Naye atokapo nje huyanena.
Marko 7:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akaendelea kusema, “Kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia unajisi. Biblia Habari Njema - BHND Akaendelea kusema, “Kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia unajisi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akaendelea kusema, “Kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia unajisi. Neno: Bibilia Takatifu Akaendelea kusema, “Kile kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Neno: Maandiko Matakatifu Akaendelea kusema, “Kile kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. BIBLIA KISWAHILI Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. |
Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo, Moyo wake hujikusanyia maovu, Naye atokapo nje huyanena.
Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka asubuhi huyafanya, sababu wana uwezo mikononi mwao.
Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu. [
Bali yeye, ambaye uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Abrahamu, akambariki yeye aliye na ile ahadi.
Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfululizo wa maumbile, nao huwashwa moto na Jehanamu.
Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?