Marko 4:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC ikawa alipokuwa akipanda, mbegu nyingine ilianguka kando ya njia, wakaja ndege wakaila. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alipokuwa akipanda mbegu, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila. Biblia Habari Njema - BHND Alipokuwa akipanda mbegu, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alipokuwa akipanda mbegu, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila. Neno: Bibilia Takatifu Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila. Neno: Maandiko Matakatifu Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila. BIBLIA KISWAHILI ikawa alipokuwa akipanda, mbegu nyingine ilianguka kando ya njia, wakaja ndege wakaila. |
Kila mtu alisikiapo neno la ufalme bila kulielewa, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.
Hawa ndio walio kando ya njia lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, mara huja Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao.
Nyingine ikaanguka penye mwamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara ikaota kwa kuwa na udongo haba;
Wale wa karibu na njia ndio wasikiao, kisha huja Ibilisi akaliondoa hilo neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka.
Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye alipokuwa akizipanda, nyingine zilianguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege wa angani wakazila.