Marko 3:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akaweka watu kumi na wawili, wapate kuwa pamoja naye, na kwamba awatume kuhubiri, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema naye akawateua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume, wakae naye, awatume kuhubiri Biblia Habari Njema - BHND naye akawateua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume, wakae naye, awatume kuhubiri Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza naye akawateua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume, wakae naye, awatume kuhubiri Neno: Bibilia Takatifu Akawachagua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume, ili wapate kuwa naye, na awatume kwenda kuhubiri Neno: Maandiko Matakatifu Akawachagua kumi na wawili, ambao aliwaita mitume, ili wapate kuwa pamoja naye, na awatume kwenda kuhubiri BIBLIA KISWAHILI Akaweka watu kumi na wawili, wapate kuwa pamoja naye, na kwamba awatume kuhubiri, |
Na mitume wakakusanyika mbele ya Yesu; wakampa habari za mambo yote waliyoyafanya, na mambo yote waliyoyafundisha.
na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.
Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lolote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na kote katika Yudea, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Paulo, mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu),