Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu; Na jamaa zangu wanasimama mbali.
Marko 14:50 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndipo wakamwacha, wakakimbia wote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia. Biblia Habari Njema - BHND Hapo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia. BIBLIA KISWAHILI Ndipo wakamwacha, wakakimbia wote. |
Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu; Na jamaa zangu wanasimama mbali.
Nilikanyaga shinikizoni peke yangu; Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami; Naam, niliwakanyaga kwa hasira yangu, Niliwaponda kwa ghadhabu yangu; Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao, Nami nimezichafua nguo zangu zote.
Yesu akawaambia, Mtakunguwazwa ninyi nyote kwa ajili yangu usiku huu; kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo watatawanyika.
Kila siku nilikuwa mbele yenu hekaluni nikifundisha, msinikamate; lakini haya yamekuwa ili maandiko yapate kutimia.
Tazama, saa inakuja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; lakini mimi siko peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.
Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao.
Katika utetezi wangu wa kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo.