Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya BWANA; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.
Malaki 4:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Angalieni, nitawatumia Eliya nabii, kabla siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogofya haijafika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Tazama, kabla ya kufika siku ile kuu na ya kutisha, nitamtuma nabii Elia. Biblia Habari Njema - BHND “Tazama, kabla ya kufika siku ile kuu na ya kutisha, nitamtuma nabii Elia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Tazama, kabla ya kufika siku ile kuu na ya kutisha, nitamtuma nabii Elia. Neno: Bibilia Takatifu “Tazama, nitawapelekea nabii Ilya kabla ya kuja siku ile iliyo kuu na ya kutisha ya Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu “Tazama, nitawapelekea nabii Ilya kabla ya kuja siku ile iliyo kuu na ya kutisha ya bwana. BIBLIA KISWAHILI Angalieni, nitawatumia Eliya nabii, kabla siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogofya haijafika. |
Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya BWANA; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.
Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya BWANA iliyo kuu na itishayo.
Hiyo siku ya BWANA iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya BWANA; Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko!
Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijia katika hekalu lake ghafla; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema BWANA wa majeshi.
Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuri; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotayarishwa.
Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.
Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?