Luka 9:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alipokuwa akisali, sura yake ilibadilika, mavazi yake yakawa meupe na kungaa sana. Biblia Habari Njema - BHND Alipokuwa akisali, sura yake ilibadilika, mavazi yake yakawa meupe na kungaa sana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alipokuwa akisali, sura yake ilibadilika, mavazi yake yakawa meupe na kung'aa sana. Neno: Bibilia Takatifu Alipokuwa akiomba, sura ya uso wake ikabadilika, nayo mavazi yake yakametameta kama miali ya radi. Neno: Maandiko Matakatifu Alipokuwa akiomba, sura ya uso wake ikabadilika, nayo mavazi yake yakametameta kama mwanga wa umeme wa radi. BIBLIA KISWAHILI Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta. |
Maana alikuwa mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.
akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
Baada ya hayo akawatokea wawili miongoni mwao, akiwa na sura nyingine; nao walikuwa wakitembea njiani kwenda mashambani.
Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka;
Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu.
Ikawa alipokuwa akisali kwa faragha, wanafunzi wake walikuwapo pamoja naye, akawauliza, Je! Makutano hao wanasema ya kuwa mimi ni nani?
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Watu wote walioketi katika ile baraza wakamkazia macho yao, wakamwona uso wake kuwa kama uso wa malaika.
Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.