Wewe nenda zako, ule chakula chako kwa furaha, unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka; kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubali kazi zako.
Luka 7:50 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akamwambia yule mwanamke, Imani yako imekuokoa, nenda zako kwa amani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye Yesu akamwambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.” Biblia Habari Njema - BHND Naye Yesu akamwambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye Yesu akamwambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.” Neno: Bibilia Takatifu Isa akamwambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.” Neno: Maandiko Matakatifu Isa akamwambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.” BIBLIA KISWAHILI Akamwambia yule mwanamke, Imani yako imekuokoa, nenda zako kwa amani. |
Wewe nenda zako, ule chakula chako kwa furaha, unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka; kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubali kazi zako.
Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake.
Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.
Yesu akamwambia, Nenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani.
Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, nenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.
Yesu aliposikia hayo alimstaajabia, akaugeukia mkutano uliokuwa ukimfuata, akasema, Nawaambia, hata katika Israeli sijaona imani kubwa namna hii.
Jiangalieni basi jinsi msikiavyo; kwa kuwa mwenye kitu atapewa, na yule asiye na kitu atanyang'anywa hata kile ambacho anadhaniwa kuwa nacho.
kwa kuwa binti yake yu karibu kufa, ambaye ni mwana pekee, umri wake amepata miaka kumi na miwili. Na alipokuwa akienda makutano walimsonga.
Ndipo Eli akajibu, akasema, Nenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.