Mfalme akajibu, akamwambia yule mtu wa Mungu, Umsihi sasa BWANA, Mungu wako, ukaniombee, ili nirudishiwe mkono wangu tena. Yule mtu wa Mungu akamwomba BWANA mkono wa mfalme ukarudishwa tena, ukawa kama ulivyokuwa kwanza.
Luka 6:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale wanaowatendea vibaya. Biblia Habari Njema - BHND Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale wanaowatendea vibaya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale wanaowatendea vibaya. Neno: Bibilia Takatifu Wabarikini wale wanaowalaani, waombeeni wale wanaowatendea mabaya. Neno: Maandiko Matakatifu Wabarikini wale wanaowalaani, waombeeni wale wanaowatendea mabaya. BIBLIA KISWAHILI wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi. |
Mfalme akajibu, akamwambia yule mtu wa Mungu, Umsihi sasa BWANA, Mungu wako, ukaniombee, ili nirudishiwe mkono wangu tena. Yule mtu wa Mungu akamwomba BWANA mkono wa mfalme ukarudishwa tena, ukawa kama ulivyokuwa kwanza.
Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa Wafilisti wametenda mambo kwa kujilipiza kisasi, nao wamejilipiza kisasi kwa moyo wa ujeuri, ili kupaangamiza kwa uadui wa daima;
basi Bwana MUNGU asema hivi; Hakika kwa moto wa wivu wangu nimenena juu ya mabaki ya mataifa, na juu ya Edomu yote, waliojiandalia nchi yangu kuwa milki yao, kwa furaha ya mioyo yao yote, kwa ujeuri wa roho zao, wakatwaa nchi yangu kuwa milki yao, kwa sababu ya malisho yake, ili kuipora;
Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.
Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi,
Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye Juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.
Hata palipotokea shambulio la watu wa Mataifa na Wayahudi pamoja na wakubwa wao juu yao, kuwatenda jeuri na kuwapiga kwa mawe,
Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona kitendo cha kuuawa kwake kuwa sawa.
kisha twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twastahimili;
Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.
watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.