Luka 24:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulubisha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Makuhani na watawala wetu walimtoa ahukumiwe kufa, wakamsulubisha. Biblia Habari Njema - BHND Makuhani na watawala wetu walimtoa ahukumiwe kufa, wakamsulubisha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Makuhani na watawala wetu walimtoa ahukumiwe kufa, wakamsulubisha. Neno: Bibilia Takatifu Viongozi wa makuhani na viongozi wetu walimtoa ahukumiwe kufa, nao wakamsulubisha. Neno: Maandiko Matakatifu Viongozi wa makuhani na viongozi wetu walimtoa ahukumiwe kufa, nao wakamsulubisha. BIBLIA KISWAHILI tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulubisha. |
Nao wakuu wa makuhani na wazee wakawashawishi makutano ili wamtake Baraba, na kumwangamiza Yesu.
Mara kulipokuwa asubuhi wakuu wa makuhani walifanya shauri pamoja na wazee na waandishi na baraza nzima, wakamfunga Yesu, wakamchukua, wakamleta mbele ya Pilato.
Kulipokucha, walikutanika jamii ya wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, wakamleta katika baraza yao, wakisema,
mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulubisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua;
ambao walimwua Bwana Yesu, na hao manabii, na kutuudhi sisi; wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wowote;