Hakika baada ya kukugeukia kwangu, nilitubu; na baada ya kufundishwa kwangu, nilijipiga pajani; nilitahayarika, naam, nilifadhaika, kwa sababu niliichukua aibu ya ujana wangu.
Luka 23:48 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na makutano yote ya watu waliokuwa wamekutanika kutazama mambo hayo, walipoona yaliyotendeka, wakaenda zao kwao, wakijipigapiga vifua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wale wote waliokuwa wamekusanyika hapo kwa ajili ya tukio hilo, walipoona hayo yaliyotukia, walirudi makwao wakijipiga vifua kwa huzuni. Biblia Habari Njema - BHND Watu wale wote waliokuwa wamekusanyika hapo kwa ajili ya tukio hilo, walipoona hayo yaliyotukia, walirudi makwao wakijipiga vifua kwa huzuni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wale wote waliokuwa wamekusanyika hapo kwa ajili ya tukio hilo, walipoona hayo yaliyotukia, walirudi makwao wakijipiga vifua kwa huzuni. Neno: Bibilia Takatifu Watu wote waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hili walipoyaona hayo, wakapigapiga vifua vyao kwa huzuni na kwenda zao. Neno: Maandiko Matakatifu Watu wote waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hili walipoyaona hayo, wakapigapiga vifua vyao kwa huzuni na kwenda zao. BIBLIA KISWAHILI Na makutano yote ya watu waliokuwa wamekutanika kutazama mambo hayo, walipoona yaliyotendeka, wakaenda zao kwao, wakijipigapiga vifua. |
Hakika baada ya kukugeukia kwangu, nilitubu; na baada ya kufundishwa kwangu, nilijipiga pajani; nilitahayarika, naam, nilifadhaika, kwa sababu niliichukua aibu ya ujana wangu.
Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipigapiga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
Na watu wote walikuwa wakilia na kumwombolezea; akasema, Msilie, hakufa huyu, bali amelala usingizi tu.
Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?