Luka 22:63 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na wale watu waliokuwa wakimshika Yesu walimfanyia dhihaka, wakampiga. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wale watu waliokuwa wanamchunga Yesu, walimpiga na kumdhihaki. Biblia Habari Njema - BHND Wale watu waliokuwa wanamchunga Yesu, walimpiga na kumdhihaki. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wale watu waliokuwa wanamchunga Yesu, walimpiga na kumdhihaki. Neno: Bibilia Takatifu Watu waliokuwa wanamlinda Isa wakaanza kumdhihaki na kumpiga. Neno: Maandiko Matakatifu Watu waliokuwa wanamlinda Isa wakaanza kumdhihaki na kumpiga. BIBLIA KISWAHILI Na wale watu waliokuwa wakimshika Yesu walimfanyia dhihaka, wakampiga. |
BWANA, mkombozi wa Israeli, Mtakatifu wake, amwambia hivi yeye anayedharauliwa na wanadamu; yeye anayechukiwa na taifa hili; yeye aliye mtumishi wao watawalao; Wafalme wataona, watasimama; wakuu nao watasujudu; kwa sababu ya BWANA aliye mwaminifu, Mtakatifu wa Israeli aliyekuchagua.
Kama vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu yeyote, na umbo lake zaidi ya wanadamu),
Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.
Basi aliposema hayo, mtumishi mmojawapo aliyesimama karibu alimpiga Yesu kofi akisema, Wamjibu hivi Kuhani Mkuu?
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.
Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.