Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa watumishi wake, aliyemwia dinari mia; akamkamata, akamkaba koo, akisema, Nilipe unachodaiwa.
Luka 20:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nionesheni dinari. Ina sura na anwani ya nani? Wakamjibu, Ya Kaisari. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Nionesheni sarafu. Je, sura na chapa ni vya nani?” Biblia Habari Njema - BHND “Nionesheni sarafu. Je, sura na chapa ni vya nani?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Nionesheni sarafu. Je, sura na chapa ni vya nani?” Neno: Bibilia Takatifu “Nionesheni dinari. Je, sura hii na maandishi haya yaliyo juu yake ni vya nani?” Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” Neno: Maandiko Matakatifu “Nionyesheni dinari. Je, sura hii na maandishi haya yaliyoko juu yake ni vya nani?” BIBLIA KISWAHILI Nionesheni dinari. Ina sura na anwani ya nani? Wakamjibu, Ya Kaisari. |
Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa watumishi wake, aliyemwia dinari mia; akamkamata, akamkaba koo, akisema, Nilipe unachodaiwa.
Naye alipokwisha kupatana na wafanya kazi kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu.
Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu.
Wakaanza kumshitaki, wakisema, Tumemwona huyu akipotosha taifa letu, na kuwazuia watu wasimpe Kaisari kodi, akisema kwamba yeye mwenyewe ni Kristo, mfalme.
Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alipokuwa mtawala wa Yudea, na Herode mfalme wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania mfalme wa Abilene,
Na tulipokusanyika akasimama mmoja wao, jina lake Agabo, akaonesha kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima, nayo ikatukia katika siku za Klaudio.
Agripa akamwambia Festo, Mtu huyo angeweza kufunguliwa, kama asingalitaka rufani kwa Kaisari.