Basi wakafanya haraka, kila mtu akalitwaa vazi lake, na kulitia chini yake juu ya madaraja, wakapiga baragumu wakasema, Yehu ni mfalme.
Luka 19:36 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na alipokuwa akienda walitandaza nguo zao njiani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akaendelea na safari, na watu wakatandaza mavazi yao barabarani. Biblia Habari Njema - BHND Yesu akaendelea na safari, na watu wakatandaza mavazi yao barabarani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akaendelea na safari, na watu wakatandaza mavazi yao barabarani. Neno: Bibilia Takatifu Alipokuwa akienda, watu wakatandaza mavazi yao barabarani. Neno: Maandiko Matakatifu Alipokuwa akienda akiwa amempanda, watu wakatandaza mavazi yao barabarani. BIBLIA KISWAHILI Na alipokuwa akienda walitandaza nguo zao njiani. |
Basi wakafanya haraka, kila mtu akalitwaa vazi lake, na kulitia chini yake juu ya madaraja, wakapiga baragumu wakasema, Yehu ni mfalme.
Watu wengi katika ule mkutano wakatandaza nguo zao njiani; na wengine wakakata matawi ya miti, wakayatandaza njiani.
Na alipokuwa amekaribia mteremko wa mlima wa Mizeituni, kundi zima la wanafunzi wake walianza kufurahi na kumsifu Mungu kwa sauti kuu, kwa ajili ya matendo yote ya uwezo waliyoyaona,