Luka 18:38 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akapiga kelele, akisema, Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye akapaza sauti akisema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!” Biblia Habari Njema - BHND Naye akapaza sauti akisema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye akapaza sauti akisema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!” Neno: Bibilia Takatifu Akapaza sauti, akasema, “Isa, Mwana wa Daudi, nihurumie!” Neno: Maandiko Matakatifu Akapaza sauti, akasema, “Isa, Mwana wa Daudi, nihurumie!” BIBLIA KISWAHILI Akapiga kelele, akisema, Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu. |
Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.
Tazama siku zinakuja, asema BWANA, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi.
Na tazama, mwanamke Mkanaani wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
Lakini wakuu wa makuhani na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto waliopaza sauti zao hekaluni, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi! Walikasirika,
Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.
Yesu alipokuwa akipita kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Mwana wa Daudi.
Basi wale waliotangulia wakamkemea ili anyamaze; lakini yeye alizidi sana kupaza sauti, Ee Mwana wa Daudi, unirehemu.
Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzawa wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.