Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Luka 18:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Yesu alipoona vile alisema, Kwa shida gani wenye mali watauingia ufalme wa Mungu!

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Yesu alipoona akihuzunika hivyo, akasema, “Jinsi gani ilivyo vigumu kwa matajiri kuingia katika ufalme wa Mungu!

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Yesu alipoona akihuzunika hivyo, akasema, “Jinsi gani ilivyo vigumu kwa matajiri kuingia katika ufalme wa Mungu!

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Yesu alipoona akihuzunika hivyo, akasema, “Jinsi gani ilivyo vigumu kwa matajiri kuingia katika ufalme wa Mungu!

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Isa akamtazama, akasema, “Tazama jinsi ilivyo vigumu kwa tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu!

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Isa akamtazama, akasema, “Tazama jinsi ilivyo vigumu kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa Mwenyezi Mungu!

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Yesu alipoona vile alisema, Kwa shida gani wenye mali watauingia ufalme wa Mungu!

Tazama sura
Tafsiri zingine



Luka 18:24
18 Marejeleo ya Msalaba  

Maana mdhalimu hujisifia tamaa ya nafsi yake, Na mwenye choyo humkana BWANA na kumdharau.


Azitegemeaye mali zake ataanguka; Mwenye haki atasitawi kama jani.


Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu; Ni kama ukuta mrefu katika mawazo yake.


Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, BWANA ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.


Ee kizazi litazameni neno la BWANA. Je! Nimekuwa jangwa kwa Israeli? Au nchi yenye giza kuu? Mbona watu wangu wanasema, Sisi tumetoroka, hatutaki kuja kwako tena?


nitawaendea watu wakubwa, nami nitasema nao; kwa maana hao wanaijua njia ya BWANA, na hukumu ya Mungu wao. Bali hawa kwa nia moja wameivunja nira, na kuvikata vifungo.


Mfalme akahuzunika sana, lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya hao walioketi karamuni, hakutaka kumkatalia.


Lakini aliposikia hayo alihuzunika sana, maana alikuwa na mali nyingi.