Luka 13:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Saa ile ile Mafarisayo kadhaa walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati huohuo, Mafarisayo na watu wengine walimwendea Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende mahali pengine, kwa maana Herode anataka kukuua.” Biblia Habari Njema - BHND Wakati huohuo, Mafarisayo na watu wengine walimwendea Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende mahali pengine, kwa maana Herode anataka kukuua.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati huohuo, Mafarisayo na watu wengine walimwendea Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende mahali pengine, kwa maana Herode anataka kukuua.” Neno: Bibilia Takatifu Wakati huo huo baadhi ya Mafarisayo wakamwendea Isa na kumwambia, “Ondoka hapa uende mahali pengine kwa maana Herode anataka kukuua.” Neno: Maandiko Matakatifu Wakati huo huo baadhi ya Mafarisayo wakamwendea Isa na kumwambia, “Ondoka hapa uende mahali pengine kwa maana Herode anataka kukuua.” BIBLIA KISWAHILI Saa ile ile Mafarisayo kadhaa walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua. |
Maana Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga, akamtia gerezani, kwa ajili ya Herodia, mke wa Filipo nduguye.
Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti ya Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode.
Na alipopata habari ya kuwa yu chini ya mamlaka ya Herode, alimpeleka kwa Herode, kwa kuwa yeye naye alikuwapo Yerusalemu siku zile.
Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alipokuwa mtawala wa Yudea, na Herode mfalme wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania mfalme wa Abilene,
Na Herode mfalme akasikia habari za yote yaliyotendeka, akafadhaika kwa sababu watu wengine walisema ya kwamba Yohana amefufuka katika wafu,