nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Luka 1:72 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ili kuwatendea rehema baba zetu, Na kulikumbuka agano lake takatifu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alisema atawahurumia wazee wetu, na kukumbuka agano lake takatifu. Biblia Habari Njema - BHND Alisema atawahurumia wazee wetu, na kukumbuka agano lake takatifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alisema atawahurumia wazee wetu, na kukumbuka agano lake takatifu. Neno: Bibilia Takatifu ili kuonesha rehema kwa baba zetu na kukumbuka agano lake takatifu, Neno: Maandiko Matakatifu ili kuonyesha rehema kwa baba zetu na kukumbuka Agano lake takatifu, BIBLIA KISWAHILI Ili kuwatendea rehema baba zetu, Na kulikumbuka agano lake takatifu; |
nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia.
Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu.
Walakini nitalikumbuka agano langu nililolifanya pamoja nawe, katika siku za ujana wako, nami nitaweka imara agano la milele pamoja nawe.
Basi, nilipopita karibu nawe, nikakutazama; tazama, wakati wako ulikuwa wakati wa upendo; nikatandika upindo wa vazi langu juu yako, nikakufunika uchi wako; naam, nilikuapia, nikafanya agano nawe, asema Bwana MUNGU, ukawa wangu.
ndipo nitakapokumbuka agano langu pamoja na Yakobo, tena agano langu na Isaka, tena agano langu na Abrahamu nitalikumbuka; nami nitaikumbuka nchi hiyo.
Wewe utamtimilizia Yakobo kweli yako, na Abrahamu rehema zako, ulizowaapia baba zetu tangu siku za kale.
Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu.
ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake;